MKENYA Karan Patel hatimaye amepata ushindi wake wa kwanza kwenye Mbio za Magari nchini Kenya (KNRC) baada ya kubeba taji la KCB Voi Rally katika kaunti ya Taita-Taveta mnamo Agosti 7.

 

Patel, ambaye alikuwa amefeli katika majaribio 40 ikiwemo kujiuzulu karibu 15 tangu shindano lake la kwanza mnamo Aprili 2014, alishinda mikondo minne kati ya nane ya Voi Rally iliyojumuisha kilomita 445.97.

 

 

 

Soma zaidi: Taifa

 

Patel aliponea chupuchupu kusalimu mari mapema katika mkondo wa kwanza wa Teita1 akiukamilisha kwa muda wa kasi ya nne-bora akiendesha gari lake la Ford Fiesta R5.

 

Baldev Chager, ambaye alikuwa akipeleka gari la Volkswagen Polo R5 linalomilikiwa na dereva Onkar Rai kwa mara ya kwanza, aliridhika na nafasi ya pili.

 

Bingwa wa duru za Afrika za Equator Rally (Kenya) na Oryx Energies (Tanzania) Carl Tundo alimaliza katika nafasi ya tatu akishirikiana na mwelekezi wake Tim Jessop katika gari la gari la Mitsubishi Evo X. Jasmeet Chana (Mitsubishi Evo X) na Aakif Virani (Skoda R5) walifunga mduara wa tano-bora. Duru hiyo ilikuwa ya nne.


Discover more from Magari Poa

Subscribe to get the latest posts sent to your email.