Oil ni kilainishi muhimu sana ndani ya gari lako, ambacho husaidia kwenye utunzaji mzuri wa injini na vyuma mbalimbali vilivyomo ndani ya gari . Mfano, Oil husaidia kulainisha sehemu za injini, kupunguza msuguano kwenye vyuma, inasafisha na kulinda injini isishike au kupatwa na kutu.
Kuna aina mbalimbali za Oil ambazo kila moja imetengenezwa kulingana na matumizi yake katika hali tofauti za kimazingira.
Mfano Oil kama :
• MINERAL OIL– Ni aina ya oil ambayo inapatikana kutokana na crude oil, hudumu kwa muda mrefu ila huchagua baadhi ya mazingira
• SYNTHETIC OIL– ni aina ya oil ambayo inatengenezwa viwandani, Oil hii imeongezewa chemicals ambazo zinaifanya iweze kumudu mazingira ya aina yoyote na kudumu kwa muda mrefu. Hii huifanya ziwe ni Oil zenye gharama kuliko Oil nyingine zote.
• SEMI-SYNTHETIC OIL– Ni aina nyingine ya Oil ambayo imetengenezwa kwa mchanganyiko wa Mineral Oil na Synthetic Oil. Hii inatoa ulinzi imara wa injini na ufanyaji mzuri wa kazi.

OIL VISCOSITY

Hii inaelezea ule mnato, utelezi au uzito uliopo kwenye mafuta, wepesi wa mafuta kumiminika kirahisi katika hali yoyote ya kimazingira Shirika la kimataifa la mainjinia wa vyombo vya moto ( SOCIETY OF AUTOMOTIVE ENGINEERS )wametofautisha mafuta kulingana na Viscosity yake. Mfano, 5W-30, 5W-40, 5W50, 0W-20 n.k
UMUHIMU WA OIL KWENYE INJINI ZA MAGARI.
• Husaidia kulainisha vyuma kwenye injini na sehemu zingine zenye vyuma.
• Husaidia kupooza joto lililopo ndani ya injini.
• Husaidia kusafisha vumbi, na mabaki yaliyotokana na milipuko ndani ya injini (combustion).
• Husaidia injini kudumu kwa muda mrefu.
• Injini yenye Oil safi hufanya kazi vizuri na kwa haraka zaidi.
• Husaidia kupunguza ulaji mbaya wa mafuta
Baada ya hiyo elimu fupi juu ya oil za magari, inashauriwa kubadilisha oil kila baada ya miezi 3 had 6 au kulingana na kilomita ulizotembea, mfano kila baada ya gari kutembea kilomita 3000 hadi 5000. Na kwa magari mapya au ya zamani yaliyotembea zaidi ya kilomita 100000 inashauriwa watumie mafuta aina ya High mileage Oil ambayo inapunguza uchomaji mbaya wa mafuta.
Kuifanyia service gari lako kwa wakati sahihi itasaidia kulifanya lidumu kwa kiwango cha ubora wake ule ule kwa muda mrefu bila shida au changamoto yoyote ndani ya injini.

Source:  Wats Ford


Discover more from Magari Poa

Subscribe to get the latest posts sent to your email.